Kufanyakazi na TPA
Bandari za Tanzania zinapirikapirika ambapo takribani watu 3,000 kila siku hufanya shughuli mbalimbali. Utekelezaji wa mradi mbalimbali kama vile ujenzi wa gati jipya (ro-ro) chini ya mradi wa lango la kuingizia meli Dar es Salaam (DMGP), gati jipya Bandari ya Mtwara, kituo kipya cha bomba la mafuta eneo la Chongoleani chini ya mradi wa bomoba la mafuta kuanzia Uganda (Hoima) mpaka Tanga (Chongoleani) na ujenzi wa bandari mpya ya pangani itaanzisha ajira nyingi mpya miaka ijayo.
Bandari za TPA zinatoa fursa nyingi. Iwapo unataka kufanyakazi za tenknolojia, fedha na mawasiliano, nahodha wa majini au katika logistiki, bandari za TPA zimejaa fursa nyingi na mbalimbali kwa ajili yako:
Wadau wengi wa bandari katika jumuiya ya Bandarini kama vile mawakala wa upokeaji na usafirishaji shehena, kampuni za meli na wasafirishaji nao pia huajiri wafanyakazi kupitia kampuni za ajira au mchakato wa kuajiri waliokazini. Zifuatazo ni baadhi ya ajira unazoweza kuomba iwapo unataka kufanyakazi katika mazingira ya bandari siku zijazo.
- Ubaharia
- Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
- Ulinzi
- Ukaguzi
- Fedha
- Mawasiliano ya Kampuni
- · Usimamizi wa kodi
- Umeme
- Ujenzi
- Wakaguzi wa Meli
- Ufundi mitambo
- Moto na Usalama
- Haidrografiki
- Utabibu
- Rasilimali watu
- Sheria
- Bima
- Masoko
- Usimamizi/Utawala wa biashara
- Upokeaji na usafirishaji shehena/li>