Mchakato wa Kupeleka Bidhaa Nje

Mizigo inayosafirishwa kwenda nje, hufikishwa bandarini, kukaguliwa na kupewa hati za ruhusa ikiwamo ya forodha. Baada ya kukamilika kwa ukaguzi na kupatikana kwa hati husika za ruhusa, mzigo hupakiwa katika vyombo husika pamoja nyaraka zote muhimu na kusafirishwa kwenda eneo ambalo limekusudiwa na msafirishaji.

Maandalizi ya Nyaraka

Jambo la kwanza, ni kwa mteja kuchagua Wakala wa Forodha na Usafirishaji (CFA) aliyesajiliwa na Mamlaka ya Kodi Tanzania na kumkabidhi nyaraka zote muhimu, huku akihifadhi nakala zake.

Baada ya CFA kukamilisha mchakato wa usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi na kupakia nyaraka kwenye mfumo wa Mamlaka ya Kodi Tanzania unaojulikana kama TANCIS, atapata hati ya ushuru wa forodha inayoruhusu kusafirisha mizigo na pia kupata ruksa (RO) kutoka TRA inayoruhusu mzigo kusafirishwa. kutoka TRA.

Malipo ya Gharama za Bandari

Wakala wa Forodha na Usafirishaji (CFA) atawasilisha Hati ya Agizo la Usafirishaji Shehena, Hati ya Ruhusa (RO) iliyotolewa na Mamlaka ya Kodi ya Mapato (TRA) na Kibali cha Kupakia Shehena kwa Ofisi Kuu ya Usafirishaji Shehena Nje ya Nchi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa ajili ya kutengeneza ankara ya malipo.

Baada ya hatua hizo malipo ya gharama za bandari yanakamilishwa.

Utambulisho wa Lori la Mizigo

Wakala (CFA) huingiza utambulisho wa lori husika katika mfumo wa mizigo na kupata Kibali cha Kuingia Bandarini.

Uwasilishaji na Upakiaji wa Shehena

Mizigo inasafirishwa hadi bandarini na kupakiwa kwenye meli husika tayari kusafirishwa kupelekwa eneo lililokusudiwa.