Bandari ya Dar es Salaam
Bandari ya Dar es Salaam
Bandari ya Dar es salaam ni bandari kuu nchini Tanzania yenye uwezo wa kuhudumia tani za metriki milioni 14 za shehena kavu na tani za metriki milioni 6.0 za vimiminika. Bandari hii ina jumla ya urefu wa meta 2,600 na gati 11 zenye kina kirefu.
Bandari ya Dar es Salaam inahudumia takriban asilimia 95% ya biashara ya kimataifa ya Tanzania. Bandari hii pia inahudumia nchi zisizo na bandari kama vile Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Malawi, Uganda na Zimbabwe.
Bandari hii ipo kimkakati ili kutumika kama kiunganishi rahisi cha usafirishaji sio tu kwenda na kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, bali pia kwenda na kutoka Mashariki ya Mbali na Kati, Ulaya, Australia na Amerika.
Sifa Bainifu za Bandari
SIFA BAINIFU | DAR ES SALAAM |
---|---|
Ukubwa wa Bandari (Mita za Mraba) | 1,090,000 |
Kina cha Maji (Mita) | 14.5m |
Uwezo wa Bandari (MT) | -- |
Idadi ya Gati | Gati 12, Gati 2 za mafuta na 1 SPM |
Urefu wa Gati (Mita) | 2,600 |
Uhimilifu Kina cha maji (Mita) | 14.5 kwa gati 0 - 7 |
Uhimilifu Kina cha maji (Mita) | 13.5 kwa gati 8 - 11 |
Urefu wa Meli Unaopokewa (Mita) | 305 |
Uzito wa Jumla wa Meli GRT | Tani za metriki 70,000 |