Bandari ya Tanga

Bandari hii iliyopo pwani ya Kaskazini mwa Tanzania ina historia ndefu.Ilijengwa mwaka 1914 kwa lengo la kutoa huduma ya biashara na kilimo kwa maeneo ya kaskazini ya Tanzania. Bandari hii kongwe zaidi nchini inaunganishwa kwa upande wa Kusini na Bandari ya Dar es salaam kwa Barabara yenye urefu wa kilometa 354. 

Sifa Bainifu za Bandari

SIFA BAINIFU TANGA
UKUBWA (Mita za Mraba) 170,000
Kina (Mita) 13
Uwezo (Tani za Metriki) 3,000,000
NYENZO
GATI
Idadi ya Gati 2
Urefu (Mita) 450
Kina (Mita) 13
HIFADHI
Idadi ya Maghala ya Hifadhi  
Ukubwa wa Eneo la Hifadhi (Mita za Mraba) 42,800
Uwezo wa hifadhi kwa Mwaka (Metriki Tani Milioni) 3
Kituo cha Kuhifadhi Magari (Mwambani) (Mita za Mraba) 60,000
Kituo cha Kuhifdhi Nafaka (Tani)  
Bandari Kavu ya Kuhifadhia Makasha  
Mfumo wa Kutia Nanga Ufukweni  
Gati ya Mafuta (Tani za Metriki) (Raskazone) 300,000
Kituo Cha Mafuta Ghafi Chongoleani (Kinajengwa)  
VIFAA (Idadi)
Mfumo Wa Kuwezesha Upakuaji Mafuta Na Gesi Kutoka Baharini (CBM) 2
Winchi za Bandarini (Uwezo wa Tani 63 Hadi 100) 5
Mitambo ya Kubeba Makasha Yenye Uzito Wa Tani 40 (aina ya Reach Stacker) 3
Mitambo Wa Kuhamishia Makasha Yasiyokuwa Na Kitu Tani 7 (Wheel Loader)  ( 7 Tani) 2
Vituo vya Kuingia na Kutoka 2
Foko Za Kubeba Mizigo Mizito (Tani 16, 25, 50) 3
Matrekta (TT) ya Kusaidia Kuhamisha Mizigo Bandarini 7
Skana ya Mizigo 3
Skana iliyosimikwa (Gantry) 1 na inayotembea (Mobile) 1 2
Winchi Kubwa ya Kubebea Makasha Inayotembea (RTG)  (RTG) 1
Tela za Kuhudumia Mzigo Bandarini 8
Magari ya Zimamoto 2
Mitambo ya Kubeba Makasha Matupu (Tani 12) 2
Boti ya Kusaidia Uegeshaji Meli 1
Mitambo ya Kuhudumia Mizigo ya Kichele (Hoppers) 5
Mitambo ya Kushika Na Kunyanyua Mizigo (Grabs) 7
Chelezo za Kuhamishia Mizigo 5
Boti Elekezi (Tugs) Inayosaidia Meli Kubaki Katika Njia Yake Ikielekea Kutia Nanga au Kutoka Bandarini (Tani 17 Hadi 70) 6
Matishari ya Mizigo (Kuanzia Tani 2,500 Hadi 3500) 5
Meli Ndogo ya Mizigo (Tani 600) 1
Mizani (Kuanzia Tani 40 Hadi 100) 4