Wanafunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu kutoka nchini Burundi wametembelea Bandari ya Dar es Salaam Jumatano, Aprili 24, 2019 kwa lengo la kujifunza shughuli za Bandari katika kuhudumia shehena hususani shehena ya mizigo ya Burundi.
Makamanda hao pia wamepata fursa ya kujifunza namna Bandari ilivyojidhatiti katika ulinzi wa mizigo ya wateja sambamba na kufahamani namna Bandari inavyochangia katika Maendeleo ya Uchumi wa Nchi.
Makamanda hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo la Mradi wa upanuzi wa Bandari na baadae kutembelea eneo lenye midaki (scanners) ya shehena ya Makasha Bandarini.