Na Leonard Magomba

Mhandisi Juma Kijavara ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kushika nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mhandisi Karim Mattaka.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Kijavara aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Mamlaka hiyo.

Mhandisi Kijavara aliwahi kushika nafasi ya Mkuu wa Bandari za Ziwa Nyasa, na baadae kuhamishiwa Bandari ya Mtwara; ambapo pia alikuwa Mkuu wa Bandari hiyo ambayo ni ya tatu kwa ukubwa katika Bandari za TPA zilizo katika Bahari ya Hindi.

Baada ya kuhudumu katika Bandari ya Mtwara kwa miongo kadhaa, alihamishiwa Bandari ya Dar es Salaam katika na kushika nafasi ya Mkurugenzi wa Bandari hiyo.

Mhandisi Kijavara alipandishwa cheo na kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu akitokea katika nafasi ya Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam ambayo kwasasa ipo chini ya Bw. Mrisho Mrisho.

Mwisho

o