KWA NINI UFANYE BIASHARA NA SISI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) ina fursa nyingi na uwezo mkubwa wa kuwezesha utekelezaji wa majukumu yake ya kuhudumia nchi zilizo jirani zinazohitaji msaada wa bandari kama lango la kuingia na kutoka kimataifa. TPA ina jukumu muhimu katika ukanda wa Afrika Mashariki ya kutoa huduma za bandari kwa nchi za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ( DRC), Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi.

ENEO LA KIMKAKATI

Bandari za TPA zikiwemo za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara kutokana na kuwa katika eneo la kimkakati zimekuwa bandari za Afrika Mashariki zenye umuhimu mkubwa. Kutokana na kuwepo katika eneo la kimkakati, bandari hizi ikiwamo ya Dar es salaam ni rahisi kutumika kufikia masoko kwa rahisi zaidi, salama na haraka.

MLANGO WA DUNIA

Kwa wateja wengi, Bandari ya Dar es Salaam ni mlango mkuu unaounganisha taifa la Tanzania, majirani na nchi nyingine duniani kote. Bandari za TPA zina uwezo wa kusafirisha mizigo yoyote (shehena ya jumla, shehena ya makasha, shehena ya vimiminika).

KIUNGO MADHUBUTI NA NCHI KAVU

Aina zote za bidhaa zinaweza kusafirishwa salama na haraka kutoka eneo lo lote la Afrika Mashariki, kutokana na usafiri mzuri wa barabara, reli na bomba la mafuta.

BANDARI YA KISASA

TPA na washirika muhimu (TICTS, ICD na CFS'S) tunaendelea kuwekeza katika teknolojia ya kisasa zaidi za utoaji wa huduma za bandari, kuwa na maeneo ya hifadhi zaidi na vifaa vya hali ya juu vya kupakia na kupakua na kutoa bidhaa kwa haraka na kwa ufanisi iwezekanavyo.

Kuna vifaa vya kujiendesha wenyewe na pia vituo vyetu vina winchi zinazojiendesha zenyewe zenye uwezo mkubwa. Tunaweza kuhudumia shehena katika kipindi chote cha mwaka iwe mvua jua kutokana na utayari wetu wa kuwa na maeneo ya hifadhi nchini kote.

  • Tumeimarisha mifumo ya Tehama kuwa na kasi katika huduma kisasa zaidi kwenye mizigo na vyombo
  • Kuunganishwa kwa mifumo usalama ya ISS Code kwa ajili ya matumizi ya bandari (Ikiwemo Mfumo wa CCTV, boti za doria, magari ya doria na Skana)
  • Electronic Payment (E-Malipo)
  • Enterprise Resource Planning (ERP)

TIJA YA JUU ZAIDI

Bandari zetu sasa zimejulikana kwa usalama wake, ufanisi na uaminifu. Bandari za TPA hutumia ujuzi, teknolojia ya kisasa zaidi na uzoefu kuendesha bandari. Kutokana na uwezo huo sisi hupakua na kupakia shehena kwa muda mfupi.

Uwezo wetu wa kubadilika kiutendaji unaleta ufanisi wa bandari na hili ni muhimu sana kwa wasafirishaji na faida kubwa kwetu kwani tunaweza kuwafikia saa 24 siku saba za wiki hata siku za sikukuu.

  • Kutokana na ukweli huo tunaweza kupokea na kutoa shehena moja kwa moja ( ikiwa imefungwa au kichele, bidhaa za chuma na kadhalika)
  • Bandari ya Dsm imeunganishwa na njia ya reli ya kati (TRL) na reli ya TAZARA)
  • Tija ya kuhudumia makasha: zaidi ya makasha 600 huhudumiwa katika kipindi cha saa 24 na TICTS, makasha 300 katika saa 24 kunakofanywa na TPA na tani 2,000 za mzigo mkubwa)
  • Muda wa kuhudumia meli ya makasha umepungua hadi siku 3.5 mwaka 2021)

HUDUMA ZA MELI

  • Wasafirishaji wakubwa wote wa meli hufika Bandari za TPA.
  • Vinara wa usafirishaji wa makasha kwenda maeneo mbalimbali duniani (MAERSK,MSC,CMA,CGM, DELMAS,EVERGREEN,PIL,EMIRATES,LNL,MOLSEVEN SEAS nakadhalika) hutumia bandari ya dar es salaam,.
  • Wauzaji wa magari wakubwa duniani (MITSUI OSK,NYK,EUKOR, etc).
  • Wabebaji wa mizigo mchanganyiko, mikubwa na ya vimiminika.

UWEZO WA HUDUMA

Bandari za TPA nchini kote zina uwezo mkubwa wa kushughulikia shehena na meli kutokana na teknolojia ya vifaa vya kisasa. Kufikia kipindi cha Juni 2022 bandari za TPA zilikuwa zimehudumia shehena ya tani za metriki milioni 20.665. Meli zikiwasili kwenye bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, huhudumiwa kwa kasi ili kuhakikisha wateja wanapata shehena zao kwa wakati.

Uingizaji wa bidhaa kutoka nje uliendelea kutawala soko, ikichukua asilimia 77.8 ya jumla ya shehena iliyoshughulikiwa mwaka 2021/22 wakati mauzo ya nje ilikuwa asilimia 21.8. Kwa upande mwingine, usafirishaji wa kwenda nje uliongezeka kwa asilimia 0.03.

Makasha yaliyoshughulikiwa katika bandari zilizopo baharini yalikuwa ni TEU 823,404. Shehena ya inayokwenda nje ilifikia tani za metriki milioni 7.801 mwaka 2021/22 ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.4 kutoka mwaka uliopita. Watumiaji wakubwa wa bandari ya Dar es salaam mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Zambia na Rwanda waliongeza matumizi ya bandari hiyo kwa asilimia 48,78.4 na asilimia 14.9 mtawalia.

Bandari ya Dar es Salaam iliendelea kutawala huduma miongoni mwa bandari za Tanzania kwa kuhudumia tani za metriki milioni 18.411 ambazo ni sawa na asilimia 89.1 ya mizigo yote. Bandari ya Tanga ilihudumia jumla ya tani za metriki milioni 0.891 sawa na asilimia 4.3 ya mizigo yote na bandari ya Mtwara ilihudumia jumla ya tani milioni 0.592 sawa na asilimia 2.9 ya mizigo yote. Bandari ndogo za Kilwa, Lindi na Mafia zilihudumia jumla ya tani za metriki milioni 0.116 sawa na asilimia 0.6 ya mizigo yote. Bandari za Ziwani (Mwanza, Kigoma na Kyela) kwa upande mwingine zilihudumia tani za metriki milioni 0.433, sawa na asilimia 2.1 ya mizigo yote.

MITIZAMO ENDELEVU YA TPA

Bandari zinazomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) zipo maeneo ya kimkakati na hivyo kuleta faida kwa wateja wote nchini na duniani wakiwemo wa Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) na Zambia wa urahisi wa utumiaji.

HUDUMA. ZA MIZIGO ZILIZO IMARA

Pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari kuwa na mpango wa kuwa na maendeleo endelevu ya miradi inayofanyika kuimarisha huduma za bandari ikiwamo ya Tehama na miundombinu mingine; matumizi ya bvandari yanazidi kukua kutokana na bandari hizo kuwa kwenye maeneo ambayo ni ya kimkakati na ukanda bora wa kijiografia.

BANDARI YA KAZI MBALIMBALI

Moja ya uwezo wa bandari za TPA ni uwepo na ushirikiano maridadi kati ya kampuni za usafirishaji, viwanda na makampuni za lojistiki. Kampuni hizi zina fursa nyingi za kuwa na mizigo; na huduma zinazotolewa na kampuni mbalimbali zinaongeza kutegemeana. Ndiyo maana Bandari za TPA, hasa bandari ya Dar es Salaam hujulikana kama bandari zinazowezesha shughuli mbalimbali zinazohusu upakuaji na upakiaji wa shehena kufanyika. Tunahakikisha kuwa shehena mbalimbali zinahudumiwa kwa kasi na kufika kwa wateja nchini, nchi jirani za Afrika Mashariki na duniani kwa haraka na kwa usalama. TPA inathamini uhusiano wake na wadau wake wote.