Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imechangia ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Kilindoni iliyoko Wilayani Mafia, mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya Mafia Martine Stephen Mtemo amepokea msaada huo uliowasilishwa na Meneja wa Bandari Ndogo Bw. Erasto J. Lugenge kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa na kuishukuru TPA kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Wilaya ya Mafia.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema uchumi wa Wilaya yake unategemea Sekta ya Bandari na kuiomba Mamlaka kuendelea kuisaidia Mafia ili kutatua changamoto za wananchi wake.
Pamoja na msaada huo, TPA pia ilijenga jetty ya Mafia mwaka 2007 na kuchangia madirisha ya Aluminium mwaka 2019 kwa ujenzi wa Kituo cha Afya Kirongwe wilayani Mafia