Na Leonard Magomba
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imeibuka kinara wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwenye Sekta za Umma na hivyo kukabidhiwa tuzo.
Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahala Pa Kazi.
Maonyesho hayo ambayo kwa mwaka huu yalienda na kaulimbiu "Mazingira Salama na yenye Afya Kazini ni Kanuni na Haki ya msingi mahali Pa kazi," yalifanyika katika viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro.
Wakati wa kilele cha maadhimisho hayo,Prof. Ndalichako alisema kwamba Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kusimamia masuala ya usalama na afya mahala pa kazi kwa kuwa ni haki ya msingi wa kila mfanyakazi nchini.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na wenye enye ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi alitembelea mabanda yote wakati wa maonyesho hayo.
Mwisho