Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania - TPA, tarehe 10 Mei, 2023 imewakutanisha Wadau wa shughuli za Bandari Nchini katika Semina ya kujenga uelewa kuhusu Mradi wa Upanuzi na Maboresho ya Miundombinu ya Bandari ya DSM.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa Gati maalum ya kuhudumia Meli kubwa za Kitalii, Kuboresha Miundombinu ya Gati la kuhudumia Abiria na Mizigo kwa Meli za Mwambao na Ujenzi wa Gati mpya nne za kuhudumia Makasha ( Makontena) Katika Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza katika Semina hiyo, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Ntandu Mathayo amesema Mradi huo utakapokamilika, utaongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia Shehena kutoka tani milioni 17 kufikia tani Milioni 28 kwa mwaka