Cargo Service

Bandari zetu zinauwezo mkubwa wa kuhudumia shehena mbalimbali zinazoingia na kutoka nchini kupitia bandari zetu. Tuna zana, vifaa na mitambo ya kutosha kushughulikia shehena za aina mbalimbali. Timu zetu zenye wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali wanafanya kazi saa ishirini na nne na siku saba kwa wiki kuhakikisha usalama wa shehena zinazoingia na kutoka katika bandari.

Aina za Mizigo Inayohudumiwa

01

Mzigo wa Makasha

Mzigo ulio ndani ya makasha unaosafirishwa kwa kutumia meli maalumu za makasha.

02

Nafaka na Kichele

Baadhi ya shehena hizi ni nafaka na malighafi kama makaa ya mawe. Nafaka hizo ni kama mchele, ngano, mahindi, maharage. Shehena hizi zina sifa mbili zinazofanana ambazo ni kutojazwa kwenye magunia na zinaulinganifu hivyo kuwa rahisi kushushwa au kumiminwa kwenye chombo kikubwa cha usafirishaji. Bidhaa ambazo zimekuwa zikihudumiwa kwa wingi na TPA ni kama makaa ya mawe, sukari, saruji, sodium nitrate, clinker, jasi, shaba, madini ya chuma na madini ya zinki.

03

Shehena Mchanganyiko

Hizi ni shehena zinazobebwa katika umbo la pamoja kama vile mzigo uliofungwa kwa mbao, mabegi, kufungwa pamoja kwa kamba, kuunganishwa na pia mizigo ya jumla isiyounganishwa kama magari. Bidhaa ambazo mara kwa mara hushughulikiwa na TPA ni pamoja na chuma, chuma cha pua, metali, magari na sehemu za vipuli, trela, bidhaa za kilimo, mitambo, shaba, vichwa na mabehewa ya treni na sehemu ya vipuli, mabehewa, matrekta na vipuli.

04

Vimininika

Shehena ya vimiminika ni pamoja na shehena yoyote inayobebwa kwenye matangi na meli kama vile petroli, mafuta ya taa, dizeli, gesi, mafuta ya ndege na mafuta ya kula.

Wadau

Tunafanya kazi na taasisi za serikali, kampuni za meli na benki ili kuwezesha huduma zetu kufanyika kwa urahisi kadiri inavyowekana kwa kufuata sheria na kanuni zote zinazohusu usafirishaji,uingizaji na utoaji wa shehena kupitia bandari zetu.

 

Chama cha Mawakala wa Meli Tanzania (TASAA)

 

Usalama wa meli yako wakati inapoingia kwenye bandari zetu ni kipaumbele chetu cha kwanza. Tunatoa huduma mbalimbali kwa vyombo vyote vinavyoingia kwenye Bandari ikiwamo uongozaji wa chombo na kuhakikisha kinafika gatini na kutia nanga salama. Kwa kutoa huduma zote zinazohusu bandari kwa kiwango cha kimataifa kunawezesha usalama wa chombo muda wote kinapofanya shughuli zinazohitaji huduma za bandari.

Huduma

Uongozaji Meli

Huduma ya mfumo wa safari za vyombo vya majini (VTS), uongozaji wa vyombo vya majini vinapoingia na kutoka bandarini unapatikana kwa saa 24 kwa meli aina zote.


Boti

Uvutaji Meli

Kuna vyombo vya uvutaji , ugeuzaji na uegeshaji meli gatini (Tugs) wakati wote .

  • Vikisaidia meli kuingia na kutoka kwa kutumia vyombo viwili vya kuvuta.
  • Vyombo vya kuvuta na kusukuma

Kufunga / Kufungua Kamba ya Meli

Kufunga au kufungua kamba ya meli katika gati kwa kutumia boti ambazo zinapatikana wakati wote.