

Rais wa Zimbabwe Mhe. Emmerson Mnangagwa ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA ) kwa ufanisi na ubora wa huduma za kibandari kwa Tanzania na nchi jirani ikiwemo nchi ya Zimbabwe.
Mhe. Rais Mnangagwa ametoa pongezi hizo alipotembelea Mabanda ya Washiriki wa maonesho ya 64 ya Biashara ya Kimataifa ya Zimbabwe [ZITF] yaliyofanyika mwezi Aprili 2024, Jijini Bulawayo Nchini Zimbabwe.
Akiwa katika Banda la TPA, Rais Mnangagwa alipewa maelezo ya huduma za TPA na hasa Bandari ya Dar es Salaam yaliyotolewa na Mwakilishi TPA Nchini Zimbabwe Bi. Kulthum Boma.
Mhe. Rais Mnangagwa amepongeza mipango ya TPA ya kuimarisha zaidi huduma ya usafirishaji wa shehena ya magari ya Zimbabwe kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi na Maendeleo ya Miundombinu Nchini Zimbabwe Mhe. Mha. Joy Makumbe (wa pili kushoto ), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Jijini Harare nchini Zimbabwe, tarehe 16 Oktoba, 2023.
Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe. Simon Sirro ( kushoto) na aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mha. Juma Kijavara ( kulia).