Bandari Ziwa Nyasa

Bandari kubwa zilizopo Ziwa Nyasa ni Mbamba bay na Itungi /kiwira. Bandari ya Kiwira imeanzishwa kama bandari ya shehena. Ina gati la kushukia na kupandia abiria, Bandari ya Kiwira ina mitambo ya kuhudumia shehena kama vile Winchi itembeayo, foko na Vinyakulio (grabs). Kwa sasa bandari hii ndio makazi ya Mv Ruvuma, Mv Njombe na Mv Mbeya ll zinazomilikiwa na TPA.

Program za Maendeleo

  • Kujenga gati Itungi, Mbamba Bay, Manda, Lupingu, Liuli na Matema katika Bandari ya Ziwa Nyasa.
  • Ununuzi vifaa vya kupakulia na mizani za kupimia mzigo uliopakiwa kwenye magari.

Miundombinu

  • Gati, maghala, eneo la kuhudumia abiria na maeneo ya wazi ya kuhifadhia mizigo

Vifaa vya bandarini

  • Meli mbili zenye uwezo wa kubeba uzito wa tani zametriki 1000 kila moja na meli moja ya abiria na mizigo inayoweza kusafirisha abiria 200 na mizigo ya tani za metriki 200.
  • Winchi inayotembea
  • Foko
  • Mizani

Miradi Iliyotekelezwa

  • Ukarabati wa Bandari ya Itungi
  • Utengenezaji wa maeneo ya abiria/shehena katika Bandari ya Kiwira
  • Ukarabati wa bandari ya Mbamba bay
  • Uendelezaji wa bandari ya Ndumbi
  • Ujengaji wa maeneo ya kupandia na kushukia abiria bandari mbalimbali wanakofikia.

Bandari Nyengine zilizoko ziwa nyasa

BANDARI YA MBAMBA BAY

Maelezo ya ziada

Bandari ya Mbamba bay ina Gati linalofaa kwa mizigo midogo. Bandari itaendelea kuboreshwa kutokana na kujengwa kwa meli mpya pia uendelezaji wa Ushoroba wa Mtwara (Mtwara Corridor).

BANDARI YA NDUMBI

Maelezo ya ziada

Bandari ya Ndumbi ina Gati, maghala, ofisi, eneo la wazi na sehemu ya kuhudumia abiria. Bandari ya Ndumbi imeonekana kuwa bandari muhimu sana iliyojengwa kimkakati kwa usafirishaji wa makaa ya mawe kwenda Bandari ya Kiwira na Bandari za Malawi kama vile Monkey bay na Chipoka

BANDARI YA ITUNGI

Maelezo ya ziada

Bandari ya Itungi imelengwa kuwa kituo cha abiria kitakacho shughulikia shehena ndogo ndogo. Bandari hii inagati lenye urefu wa mita 70, ni ofisi kuu ya Bandari za ziwa Nyasa. Inakadiliwa na tatizo la mchanga wa tope unaothiri njia ya kuingilia Bandarini hata hivyo utaratibu wa kudhibiti unaonesha mafanikio . Bandari ina mtambo wa kusafisha taka chini ya maji naa hivyo kuwezesha kina cha maji kuongezeka katika mkondo wa kuingilia upande wa Gati.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Meneja wa Bandari Ziwa Nyasa,
Mamlaka ya Bandari (TPA),
S.L.P 400,
Kyela, Tanzania

Simu: +255 (0) 786 364 622
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Ziwa Tanganyika

Ziwa Tanganyika lipo katika Mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Bandari kuu zilizopo katika ziwa hili ni ya Kigoma, Kibirizi, Kipili, Kasanga, Kagunga, Kabwe na Kirando. Bandari ya Kigoma imeungwa kwa barabara na reli na ina vifaa vingi vikiwemo mizani, matangi ya mafuta, karakana na eneo la kupumzikia abiria.

Sifa za Bandari ya Kigoma

  • Ndio bandari kuu ndani ya ziwa Tanganyika
  • Iko mkoa wa Kigoma
  • Kuna eneo maalumu la Shehena, Abiria na kupakulia mafuta
  • Imeunganishwa kwa barabara na reli hapa nchini nan chi za jirani

Miundombinu ya Bandari

Gati

  • Gati la Kontena la meta 100
  • Bidhaa za kawaida meta 210
  • Kituo cha abiria meta 122.7
  • Gati la bomba la mafuta meta 110

Vifaa

  • Winchi inayoendeshwa kwenye reli
  • Reach stacker
  • Foko
  • Winchi
  • Matrekta

Uhifadhi

  • Ghara Kuu
  • Mabanda

Miradi Iliyotekelezwa

  • Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Bandari katika Bandari ya Kigoma, ujenzi wa gati, ghala na eneo la kuhudumia abiria katika bandari ya Kibirizi na Ujiji kwenye Ziwa Tanganyika.

Bandari nyingine za Ziwa Tanganyika

BANDARI YA KIBIRIZI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ni bandari yenye shughuli nyingi inayohudumia abiria na mizigo kwa soko la ndani na la Jamhurti ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Burundi na Zambia. Mahali ilipo
  • Ipo kilometa 2.6 kutoka bandari ya Kigoma
Miundombinu
  • Jengo la abiria
  • Ghala la mizigo
  • Ofisi za bandari
  • Ofisi ya Wadau
Gati
  • Kuna gati kwa ajili mizigo na abiria
Miradi inayotekelezwa
  • Ujenzi wa gati, ghala na eneo la kuhudumia abiria

BANDARI YA KABWE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Rukwa kiasi cha kilometa 84 kutoka Namanyere
Gati
  • Ina gati kwa mizigo mchanganyiko
Miradi inayotekelezwa
  • Ujenzi wa eneo la kupakia na kupakua mafuta

BANDARI YA KIPILI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Rujkwa kilometa 64 kutoka Namanyere
Facilities
  • Jengo la abiria
Gati
  • Gati la mizigo mchanganyiko
Uwezo wa sasa
  • Tani 6,000
Miradi inayotekelezwa
  • Ujenzi wa barabara katika bandari ya Kipili

BANDARI YA KASANGA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Rukwa kiasi cha kilometa 110 kutoka Sumbawanga
Vifaa
  • Mobile Groove
  • Foko
Gati
  • Ujenzi wa gati la meta 14
Ghala
  • Maghala Mawil
Uwezo wa sasa
  • Tani 12,000
Miradio inayotekelezwa
  • Kuboresha bandari ya Kasanga

BANDARI YA KAGUNGA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo kilometa 120 kutoka Kigoma mjini
Miundombinu
  • Jengo la abiria
Gati
  • Mizigo mchanganyiko 50M
Hifadhi
  • Ghala moja
Uwezo wa sasa
  • Tani 6,000
Miradi inayotekelezwa
  • Ujenzi wa barabara kutoka mpakani na Burundi hadi bandari ya Kagunga

BANDARI YA LAGOSA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo kilometa 180 kutoka Kigoma
Miradi inayotekelezwa
  • Ujenzi wa gati

BANDARI YA SIBWESA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Kigoma kilometa 340 kutoka bdanri ya Ikola
Miundombinu
  • Jengo la abiria
Gati
  • Gati la mizigo mchanganyiko meta 100
Hifadhi
  • Ghala moja

BANDARI YA KAREMA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani katawi kilometa 120 kutoka Mpanda
Jengo la abiria
  • Eneo la wazi
Hifadhi
  • Ghala
Miradi unayoitekelezwa
  • Kuboresha bandari ya Karema

BANDARI YA IKOLA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Iko mkoani Katavi kilometa 10 kutoka Bandari ya Karema

BANDARI YA NINDE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo kilometa 160 kutoka bandari ya Kipili

BANDARI YA MSAMBA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Rukwa kiasi cha kilometa 250 kutoka Bandari ya Ninde

BANDARI YA WAMPEMBE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Rukwa kiasi cha kilometa 280 kutoka bandari ya Msamba

BANDARI YA KALA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo kilometa 280 kutoka bandari ya Wampembe

BANDARI YA UJIJI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 9.4 kutoka bandari ya Kigoma
Miradi unayoitekelezwa
  • Kuboresha gati ya bandari ya Ujiji

BANDARI YA KATONGA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo kilometa 3.6 kutoka Kigoma

BANDARI YA KORONGWE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Rukwa kilometa 60 kutoka bandari ya Kabwe

BANDARI YA KIRANDO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Rukwa kilometa 10 kutoka bandari ya Kipili

BANDARI YA KATOSHO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kiasi cha kilometa 4 kutoka bandari ya Kigoma

BANDARI YA TONGWE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Kigoma kiasi cha kilometa 330 kutoka barabara ya Ilagala

BANDARI YA LUBENGERA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 4.32 kutoka barabara ya Ilagala

BANDARI YA SIGUNGA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 2.3 kutoka barabara ya Ilagala

BANDARI YA HEREMBE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 2.6 kutoka barabara ya Ilagala

BANDARI YA MTANGA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 70 kutoka bandari ya Kigoma

BANDARI YA MWAMGONGO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 156 kutoka bandari ya kigoma

BANDARI YA KARAGO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 2.5 kutoka barabara ya Ilagala

BANDARI YA KAPARAMSENGA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 1.5 kutoka barabara ya Ilagala

BANDARI YA KALYA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 25 kutoka bandari ya Sibwesa

BANDARI YA RUKOMA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kigoma kilometa 2.6 kutoka barabara ya Ilagala

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Meneja wa Bandari Ziwa Tanganyika,
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
S.L.P 911,
Kigoma, Tanzania

+255 (28) 2802275
Simu 1: +255 (0) 689 949 194
Simu 2: +255 (0) 713 220 588
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Bandari ya Mtwara na nyingine za Bahari ya kusini

Bandari ya Mtwara ni miongoni mwa bandari kuu tatu zinazosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) iliyopo Kusini mwa Tanzania karibu na mpaka na Msumbiji.

Kijiografia inapatikana kilomita 578 Kusini mwa Jiji la Dar es Salaam. Bandari ya Mtwara ambayo ina kina kirefu ilijengwa kati ya mwaka 1948 na 1954. Ujenzi wa awali na uendelezaji wa bandari hiyo uliendana na ujenzi wa reli kuanzia Mtwara hadi Nachingwea.

Sifa za Bandari

Eneo la gati lina kina kirefu cha meta 9.5 hadi 13.5, hakuna masharti ya maji kupwa na maji kujaa kwa meli zinazoingia na kutoka bandarini.

Nyenzo za Bandari

Ukuta wa Gati

Bandari ina ukuta wa gati wenye urefu wa mita 385 unaoweza kutia nanga meli mbili na chombo kimoja cha mwambao kwa wakati mmoja. Kina cha meli ni mita 9.85 nakutokana na vifaa vya sasa vya kuongozea meli vinavyotumia umeme wa jua, meli zitaingia muda wote (saa 24)

Miundombinu ya Bandari

Bandari ina gati lenye urefu wa meta 385 linalowezesha meli nne kutia nanga na chombo kimoja cha mwambao kwa wakati mmoja. Bandari hii ikiwa na kina cha meta 9.5 hadi 13.5 huku ikiwa na vifaa vya kisasa vya kuongozea meli vinavyotumia umeme wa jua, meli zinaweza kuingia bandarini muda wowote katika saa 24 za siku.

Vifaa

Miundombinu ya kuhudumia shehena iliyopo ni pamoja na zana mbalimbali za kupakilia, kupakulia na kupanga. Zana hizo ni kreni kubwa ya kupakia na kupakua shehena za makasha kwenye meli (SSG), winchi inayotembea yenye uwezo wa tani 100, Reach Stacker zenye uwezo wa kubeba tani 45 kila moja, Front Loader tani 42, winchi zinazotembea zenye uwezo wa tani 50 na tani 25, mitambo ya kubeba makasha matupu,foko zinazobeba tani 16, tani 5 na tani 3 , matrekta, Hoppers na Grabs.

Kuna mashua za kusogezea meli na kuongoza (Tug Boat na Mooring Boat). Bandari ya Mtwara ina vifaa vingi na imejiandaa kuhudumia aina zote za shehena kwa saa 24 siku saba kwa wiki. Pamoja na bandari ya Mtwara zipo bandari ndogo za Lindi na Kilwa.

Maghala

Kuna ghala kuu mbili za shehena zenye jumla ya zaidi ya eneo la mraba 15,000. Hifadhi ya wazi iliyojengwa kwa jumla ya meta za mraba 124,000 ikijumuisha meta za mraba 76,000 iliyojengwa mwaka wa 2020. Hifadhi ya wazi ya meta za mraba 20,000.

Uwezo wa Sasa

Bandari ya Mtwara inaweza kuhudumia tani 1,000,000 za shehena zinazoingizwa na kusafirishwa nje kwa mwaka. Bandari hii imejengwa hasa kuhudumia bidhaa mchanganyiko na makasha.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:-

Meneja wa Bandari Mtwara,
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
S.L.P 530,
MTWARA, Tanzania

Simu. +255 (23) 2333125
Faksi +255 (23) 2333153
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 

Bandari Ziwa Victoria

Ziwa Victoria lina bandari nyingi lakini zilizo kubwa ni Mwanza Kusini na Mwanza Kaskazini ambazo zinaungwa na barabara na reli nchini na nchi jirani. Bandari hizi zina miundombinu ya kutosha, kuwezesha huduma za bandari ikiwamo mizani ya magari, matangi ya mafuta, karakana na jengo la abiria.Mbali na bandari hizi mbili Ziwa Victoria lina bandari nyingi zinazofanyakazi ya kutoa huduma kwa umma.

Sifa za Bandari

  • Bandari hizi ambazo zipo mkoani Mwanza zimeunganishwa kwa barabara na reli nchini na nchi za jirani.

Miundombinu ya bandari

Gati

Bandari zina gati la shehena ya kawaida la meta 280 na Bomba la Mafuta ambalo lipo Mwanza Kusini. Gati namba moja lina meta 82.5 ( kituo cha shehena) Gati 2– meta 60 ni kituo cha abiria wakati Gati 3 – meta 60 (jengo la abiria) na gati la meta 10 kwa kituo cha abiria Mwanza Kaskazini.

Vifaa

  • Winchi kubwa ya Bandini
  • Foko
  • Winchi itembeayo
  • Kizoa taka chini ya maji (Water Master)
  • Boti ya kuvutia / kuongozea meli Baharini
  • Gati linaloelea

Uhifadhi

Kuna mabanda matatu yaliyopo Mwanza Kusini

Bandari ziwa victoria

BANDARI YA MWANZA SOUTH

Maelezo ya ziada
Miundombinu Mizani Linkspan Karakana ya mitambo Gati Vifaa Winchi kubwa ya bandarini Foko Winchi inayiotembea Mtambo wa kutolea tope Tishari Hifadhi Kuna maghala matatu (3) ambayo yapo Bandari ya Mwanza Kusini
Tabia
  • Ipo mkoani Mwanza na maalumu kwa mizigo na mafuta na inaunganishwa nan chi jirani kwa barabara na reli.
Miundombinu
  • Mizani
  • Linkspan
  • Karakana ya mitambo
Gati
Vifaa
  • Winchi kubwa ya bandarini
  • Foko
  • Winchi inayiotembea
  • Mtambo wa kutolea tope
  • Tishari
Hifadhi
  • Kuna maghala matatu (3) ambayo yapo Bandari ya Mwanza Kusini

BANDARI YA MWANZA NORTH

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani mwanza Maalumu kwa mizigo na abiria na inaunganishwa na barabara na treni kwa Tanzania na nchi jirani
Miundombinu
  • Mizani
  • Jengo la abiria
  • Matangi ya mafuta
Gati
  • Gati la kwanza- Meta 82.5 kwa ajili ya mizigo
  • Gati la pili Meta 60 kwa ajili ya abiria
  • Gati la tatu 3 Meta 60 kwa ajil
Vifaa
  • Jenereta

BANDARI YA KEMONDO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kagera
  • Iko mahususi kwa ajili ya mizigo ya kawaida na abiria na imeungwa na mikoa nan chi jirani kwa barabara.
Miundombinu
  • Jengo la abiria
  • Linkspan
  • Maghala matano ya muda
  • Maghala ya kuhifadhia bidhaa
Gati
  • Gati la meta 22 kwa ajili ya mafuta
  • Gati la 1 – meta 70
  • Gati la 2 – meta 22
  • Gati la 3 – meta 37

BANDARI YA BUKOBA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Kegera na mahususi kwa mizigo na abiria
  • Imeungwa kwa barabara na maeneo nchini na nchi jirani
Vifaa
  • Tela za mizigo
  • Trekta/li>
Gati
  • Gati la 1 Meta 82.5
  • Gati la 2 Meta 60
  • Gati la 3 Meta 60

BANDARI YA MUSOMA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Mara na mahusisi kwa mizigo na abiria na imeunganishwa nchini nan chi jirani kwa barabarali>
Miundombinu
  • Jengo la abiria
  • Ghala
Quay Wall
  • Gati la 1 – meta 100
  • Gati la 2 – meta 60

BANDARI YA NANSIO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Mara na ni mahususi kwa abiria na mizigo ikiwa imeunganishwa nchini nan chi jirani kwa barabara
Miundombinu
  • Jengo la abiria
  • Ghala
Gati

BANDARI YA MWIGOBERO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Mara na iko mahsusi kwa mizigo na abiria ikiwa imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa barabara.
Gati
  • Gati kwa ajili ya mizigo ina meta 203

BANDARI YA SHIRATI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Mara na ni mahsusi kwa shughuli za abiria na mizigo na imeunganishwa kwa njia ya maji nchini na nchi jirani.

BANDARI YA KINESI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Mara ni kwa ajili ya abiria na mizigo,imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji .

BANDARI YA MAISOME

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Mara na ni mahususi kwa abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji .

BANDARI YA KOME

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Sengerema mkoani Mwanza na inatumika kwa ajili ya abiria na mizigo na inaunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA BUKONDO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Sengerema mkoani Mwanza ikijihusisha na mizigo na abiria na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA KAHUNDA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Geita ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA CHATO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Geita ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA NYAMIREMBE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Geita ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA NKOMBE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Geita ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA MUHARAMBA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo mkoani Geita ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA BUCHOSA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • LIpo Sengerema Mkoani Mwanza ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA SOLIMA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Busega Mkoani Simiyu ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA UKARA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Ukerewe, Mkoani Mwanza ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA NYAKALILO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Sengerema Mkoani Mwanza ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA KYAMKWIKWI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Muleba Mkoani Kagera ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA BUCHENZI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Sengerema Mkoani Mwanza ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA KARUMO

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Sengerema Mkoani Mwanza ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA ITABAGUMBA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • LIpo Sengerema Mkoani Mwanza ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA LUSHAMBA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Sengerema Mkoani Mwanza ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA LUGATA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Sengerema Mkoani Mwanza ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA NUNGWE

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Mkoani Geita ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA KIBARA

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Bunda Mkoani Mara ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.

BANDARI YA MAGARINI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Muleba Mkoani Kagera ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji..

BANDARI YA NYAMKAZI

Maelezo ya ziada
Tabia
  • Ipo Bukoba Mkoani Kagera ikihudumia abiria na mizigo na imeunganishwa nchini na nchi jirani kwa njia ya maji.
 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Meneja wa Bandari Ziwa Victoria,
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
P. O. Box 3100,
Mwanza, Tanzania

Simu 1. +255 (28) 22541422
Simu 2. +255 (0) 787 250181
Faski. +255 (28) 22541422
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
 

Bandari ya Tanga na Bandari nyingine za Bahari za Kaskazini

Bandari ya Tanga ilijengwa mwaka 1914 awali ili kuhudumia mahitaji ya kibiashara na kilimo kaskazini mwa Tanzania. Bandari ya Tanga iko katika pwani ya kaskazini mwa Tanzania. Tanga ni moja ya bandari kongwe inayomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ipo kaskazini mwa Tanzania. Bandari hii inasimamia pia bandari nyingine ndogo za Pangani, Kipumbwi, Kigombe na Mkwaja.

Bandari hii imeunganishwa vyema na barabara zinazotoka kaskazini na kati ya Tanzania na kuingia mkoani Tanga na hivyo kurahisisha usafiri kwenda mikoa hiyo na nchi jirani. Aidha bandari hii inaunganishwa upande wa kusini na bandari ya Dar es salaam kwa umbali wa kilomita 354.

Sifa za Bandari ya Tanga

Kila bandari ina sifa zake za kipekee ambazo zinachochea utendaji na ufanisi wa utoaji huduma bandarini. Zifuatazo ni baadhi ya sifa muhimu za Bandari ya Tanga.

  • Bandari hii ipo kimkakati zaidi kutokana na eneo ilipo. Yenyewe inahudumia mikoa ya kaskazini ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Kanda ya Ziwa na nchi za jirani za Rwanda, Burundi na sehemu ya kusini ya Uganda
  • Ina kina kikubwa na mlango mpana wa kutosha kuingiza meli yenye kina chochote
  • Haina kipingamizi cha maji kupwa na kujaa kwa meli zinazoingia na kutoka bandarini
  • Ina ghuba ya asili inayokinga meli hivyo kuwezesha huduma kufanyika bila hofu.

Nyenzo za Bandari

Ukuta wa Gati

Bandari ya Tanga ina ukuta wa gati la kisasa wenye urefu wa mita 381 unahusu wa kwanza na wa pili. Ukuta wa kwanza ulikuwa na urefu wa mita 240 ulijengwa mwaka 1918 na sehemu iliyobaki mwaka 1954.

Miundombinu ya Bandari

Bandari ya Tanga ina mabanda matatu yaliyoezekwa kwa ajili ya shehena zinazoathiriwa na hali ya hewa.

  • Bandari ya Tanga ina gati mbili za kisasa zenye jumla ya urefu wa mita 450. Pia kuna mabomba mawili ya inchi 12 ambayo hutumika kupakua shehena za mafuta. Mfumo wa Conventional Buoy Mooring (CBM) umewekwa katika kisiwa cha Totten kwa ajili ya kuhudumia shehena ya gesi ya kupikia, (Liquefied Petroleum – LPG-). Mfumo huu umeungwa kwa njia ya mabomba yaliyounganishwa chini ya bahari hadi nchi kavu.
  • Kuna eneo la sakafu ngumu linalopokea shenena mchanganyiko la ukubwa wa meta za mraba 29,000
  • Yapo maghala matatu yenye jumla ya ukubwa wa meta za mraba 13,800
  • Kuna eneo maalumu la matengenezo ya vyombo vya baharini (chelezo)
  • Kuna eneo la kuhudumia meli za abiria.
 

Vifaa

Uhai wa bandari unategemea vifaa vilivyopo. Bila ya vifaa hakutakuwa na shughuli za bandari. Bandari ya Tanga ina vifaa lukuki vya kuhudumia shehena za aina mbalimbali:-

  • Winchi za bandarini (Habours Mobile cranes) sita zenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 63 kila moja kwa wakati.
  • Mashua elekezi (Tugs) zinazowezesha meli kubaki katika njia yake wakati wa kutia nanga
  • Matishari yenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 3,500 kila moja
  • Cargo Lighter yenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 600
  • Pantuni za kuhamishia shehena
  • Mtambo wa kuhamishia makasha yasiyokuwa na kitu wenye uwezo wa kubeba uzito wa tani 12
  • Mitambo ya kubeba makasha yenye uzito wa tani 40
  • Matrekta (TT) ya kusaidia kuhamisha mizigo
  • Foko maalumu kwa kuhudumia marobota ya katani
  • Foko za kawaida saba
  • Foko nne zenye uwezo wa kubeba tani nne kila moja
  • Foko tatu zenye uwezo wa kubeba tani tano kila moja
  • Matela ya kuhudumia mzigo bandarini
  • Magari ya zimamoto yenye vifaa vya kukabiliana na moto
  • Boti ya kusaidia uegeshaji (Mooring Boat)
  • Mizani kwa ajili ya upimaji wa mzigo
  • Midaki ya kukagua mizigo
  • Hoppers kwa ajili ya kuhudumia mzigo wa kichele
  • Grabs kwa ajili ya kuhudumia mzigo wa kichele
 

Hifadhi

Bandari ya Tanga ina maghala matatu yaliyoezekwa kwa ajili ya shehena zinazoathiriwa na hali ya hewa.

  • Eneo lenye sakafu ngumu kwa ajili ya kuhifadhia makasha na shehena nyingine zisizohitaji kufunikwa lenye meta za mraba 29,000.
  • Maghala yaliyoezekwa yenye eneo la meta za mraba 13,800
 

Uwezo

Uwezo wa sasa wa bandari ambao umeboreshwa umewezesha kuhudumia tani 1,201,000 za shehena kwa mwaka.

 

Uboreshaji Bandari ya Tanga

Maboresho yanaendelea kwenye Bandari ya Tanga ikijumuisha kuongeza kina, kuimarisha gati namba moja na mbili na kuboresha uwezo wa kuhudumia meli na mzigo zaidi.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Meneja wa Bandari Tanga,
Mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA),
Bandari House
S.L.P 443,
Tanga, Tanzania

Simu +255 (27) 2643078
Faski: +255 (27) 2642360
Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.