Bandari kuu ya Dar es salaam ya TPA inatoa taarifa za kawaida kuhusu bandari zote. Ndiyo tunapokea wanafunzi wanapofanya mazoezi au kazi za ugani kwa makubaliano maalumu bila ya gharama yoyote kwa TPA. Kutokana na ukweli kwamba bandari zetu ni maeneo nyeti na tunapokea maombi mengi na ratiba za kazi nyingi bahati mbaya mamlaka ya bandari haiwezi kukubali maombi yote kutoka kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu.