Select your language

Wadau mbalimbali wanaohusika na shughuli za kibandari wametumia ipasavyo ushiriki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Maonesho ya 33 ya Kimataifa ya Wakulima yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt.John Malecela jijini Dodoma, kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yahusuyo sekta hiyo na Uchukuzi kwa ujumla.
Sehemu kubwa ya Wadau hao ni wakuu wa Taasisi, Wafanyabiashara, wafanyabiashara, Wasafirishaji wa mazao, malighafi na zana za kilimo.
TPA imetumia ushiriki wake katika Maonesho haya ya Wakulima kuonyesha namna inavyohudumia shehena mbalimbali na jinsi ilivyojipanga kutekelza Dira 2050 hususani katika
kichocheo cha Usafirishaji fungamanishi ambapo Serikali imeeleza dhamira yake ya kuunganisha Bandari na reli za kisasa ili kuongeza ufanisi katika sekta ya Uchukuzi nchini.