Select your language

Meli ya MV AFRICAN DIPPER yenye urefu wa mita 179.9, tarehe 10 Machi,2025, imewasili katika Bandari ya Mtwara ikitokea nchini Uturuki ikiwa na shehena ya Sulphur, tani 9,202.54 ( Elfu tisa mia mbili na mbili nukta tano nne)

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Kanali Michael Mtenjele ameongoza mapokezi ya meli hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawala ambapo ametoa wito kwa Bodi ya Korosho kuhakikisha kuwa Sulphur hiyo inasambazwa kwa wakati kwa wakulima ili kuleta tija katika uzalishaji wa zao la Korosho.

Naye Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi amesema Bandari ya Mtwara imejipanga vema kwa rasilimaliwatu ya kutosha, vitendea kazi na mitambo ili kuhudumia shehena mbalimbali ikiwemo Sulphur.