Select your language

Bandari ya Tanga imehitimisha zoezi la kufanya uchaguzi wa kuchagua Wajumbe Wawakilishi wa Idara na Wajumbe kwa ajili ya Kamati ya Utendaji ya  Baraza Dogo la Uchumi la kituo hicho. Pia walichaguliwa Wajumbe wawakilishi kwa ajili ya Baraza Kuu la TPA.

 

Akiongea katika uchaguzi huo, msimamizi wa uchaguzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi , Ajira na Mahusiano, Afisa kazi Mfawidhi wa Mkoa wa Tanga, Bi. Janeth Omolo alisema kuwa, lengo kuu la baraza hilo ni ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kutoa maamuzi, kushauri na kutatua changamoto ili kuleta ufanisi mahala pa kazi .

 

“Mabaraza haya yapo kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sheria za Taasisi za Kazi, Sheria ya Majadiliano ya pamoja, Sheria za Utumishi wa Umma pamoja na Mikataba ya Kimataifa iliyotiwa saini na Tanzania, Sheria zote hizi kwa pamoja zinasimamia mabaraza ya wafanyakazi”. Aliongeza Omolo

 

Wawakilishi hao waliochaguliwa na idara wanazotoka kwenye mabano ni; Lilian Sauwa (Rasilimali Watu), Innocent  Mark ( Fedha),  Riziki Mgude (Usaidizi Biashara na Ugavi) na Issa Abdallah ( Ulinzi).

 

Wengine ni Mathias Lyon (Marine), Joseph Mwambipile na  Bernard Malima (Utekelezaji), Twalibu Twalibu (Uhandisi) na Cliff Mkahala (Zimamoto na Uokoaji).

 

Aidha Baraza la Uchumi liliwachagua Wajumbe Bernard Malima, Mathias Lyon na Twalibu Twalibu kuingia kwenye Kamati ya Utendaji. Pia walichaguliwa   Joseph Mwambipile na Lilian Sauwa kuwa Wajumbe wa Baraza Kuu la TPA.

 

Wakati huo huo Baraza hilo liliwachagua Kelvin Ikunguru kuwa Katibu wa Baraza la Uchumi, Bandari ya Tanga na Mariam Sultan kuwa Naibu Katibu wa Baraza.