BARAZA KUU LA WAFANYA KAZI (MWC) LAFANYA KIKAO CHAKE CHA 40 MJINI MOROGORO
Baraza Kuu la Wafanyakazi (MWC) la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) tarehe 9 Septemba 2026 limefanya kikao chake cha 40 mjini Morogoro. Kikao hicho kimelenga kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 pamoja na mpango wa Bajeti iliyoidhinishwa na Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2026/ 2027. Pamoja na mambo mengine Baraza hilo pia limemuaga aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi (DOWUTA) Tawi la Makao Makuu aliyemaliza muda wa utumishi kisheria Bw. Benjamin Kihanga Kikao hicho kimeongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu (TPA) Dkt. Baraka R. Mdima kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Plasduce M. Mbossa.

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"