BARAZA LA WAFANYAKAZI LA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)

Baraza la Wafanyakazi la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kituo cha Makao Makuu limefanya kikao cha thelathini na saba (37) tarehe 14 Februari, 2025 mjini Bagamoyo, chenye lengo la kupokea taarifa ya utekelezaji wa malengo kwa mwaka wa fedha 2024/2025. kwa kipindi cha nusu mwaka (Julai - Desemba 2024) pamoja na kupokea mapendekezo ya Mpango wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Baraza hilo limeongozwa na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt. Baraka R. Mdima kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw.Plasduce M. Mbossa.