KAMATI YA (PAC) YA BARAZA LA ZANZIBAR YARIDHISHWA NA MIRADI KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi katika Bandari ya Dar es Salaam na kupongeza juhudi za Serikali ya awamu ya Sita kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya bandari, hatua inayochochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Hayo yamebainishwa na Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mwakilishi wa Jimbo la Wingwi (Pemba) kupitia chama cha ACT Wazalendo Mhe. Kombo Mwinyi Shehe, tarehe 7 Agosti 2026, mara baada ya kufanya ziara ya siku mbili katika Bandari ya Dar es salaam kujionea mandeleo ya Utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika Bandari hiyo yanayolenga kuongeza ufanisi na mapato nchini.
Pamoja na mambo mengine kamati hiyo imepata fursa ya kutembelea gati 0–7 yanayoendeshwa na DP World na gati 8-11 inayoendeshwa na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL) pamoja na kitengo cha kuhudumia mafuta (KOJ) na baadae kutembelea Mradi wa ujenzi wa matanki 15 ya kuhifadhi na kusambaza mafuta uliopo Kigamboni, Dar es Salaam.

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"