Select your language

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce M. Mbossa, tarehe 23 Machi 2026 ameongoza  Kikao cha (39) cha Kamati ya Utendaji Baraza Kuu la Wafanyakazi la (TPA) kilichofanyika Mjini Morogoro.

 

Kikao hicho kimelenga  kujadili mapendekezo ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

 

Mpango na Bajeti ya kila mwaka inaandaliwa kama mkakati Maalum wa utekelezaji majukumu ya TPA ambayo ni Kumiliki, Kusimamia, Kushirikisha sekta binafsi na Kuendeleza Bandari zote nchini.

 

Bandari hizo ni pamoja na Bandari Kuu za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, Bandari ndogo za Kilwa, Lindi, Mafia, Bagamoyo, Pangani na Bandari myingine ndogondogo  katika mwambao wa Bahari ya Hindi pamoja na Bandari za Maziwa (Ziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa).

 

Kikao cha Kamati ya Utendaji kinakutana kwa siku bili (2) kikifuatiwa na kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi kitakachofanyika tarehe 25 Machi, 2026.