Select your language

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mha. Ali Said Bakar, ametembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) katika maonesho ya maadhimisho ya siku ya Mabaharia Duniani yanayofanyika kitaifa mkoani Kigoma, katika viwanja vya Mwanga Center.Akiwa katika banda hilo, Mha. Bakar alipata maelezo mafupi kuhusu namna TPA inavyotekeleza majukumu yake pamoja na mchango wake mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania kupitia huduma za bandari na usafirishaji majini.Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohamed,Mha. Bakar aliwataka mabaharia nchini kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa nidhamu, weledi na uzalendo wanapotekeleza majukumu yao ya kibaharia ndani na nje ya nchi.Amesisitiza kuwa, lengo la maadhimisho hayo ni kujenga uelewa kwa umma kuhusu mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotolewa na mabaharia katika maendeleo ya taifa na sekta ya usafirishaji majini.