Select your language

Meneja wa Bandari ya Tanga Bw. Salehe Mbega ameongoza Kikao cha 71 cha Baraza Dogo la Majadiliano la kituo hicho (JIC) kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano ulipo katika Jengo la Bandari “Bandari House jijini Tanga.

Mbega aliwaambia wajumbe hao kuwa kwa sasa Bandari hiyo imeendelea kuhudumia shehena mbalimbali zinazotoka na kwenda nje ya nchi kama vile Magari, Malighafi za viwandani, Mitambo mbalimbali, Mkonge na shaba.

Aidha katika kikao hicho hoja mbalimbali ikiwa ni pamoja na masuala ya yanayohusu wafanyakazi na mambo ya kiutendaji ambapo hoja hizo zilijadiliwa na kupatiwa ufumbuzi.

Pia Kikao kilifanya uchaguzi wa kuchagua Sekretarieti ya Baraza hilo ambapo wajumbe walimchagua Bi. Clara Matei kuwa Katibu wa Baraza hilo na Bw. Ibrahim Nzori kuwa Katibu Msaidizi.

#tpa #bandari#port#tanga