Select your language

Konsula Mkuu wa Tanzania mjini Lubumbashi, Mhe. Magabilo I. Murobi, Mei 22, 2026 mekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mwakilishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mjini Kolwezi Mkoa wa Lualaba ulioko kusini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Bi. Kuruthum A. Ngunguti, pamoja na watendaji wa ofisi hiyo katika ofisi za TPA Mjini Kolwezi. Mazungumzo yao yalijadili changamoto mbalimbali pamoja na mikakati ya kuendelea kuimarisha biashara kati ya Tanzania na DRC kupitia Bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara na Bandari za Maziwa Makuu.