Select your language

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Mhe. Uzairu Abdul Athumani, tarehe 4 Juni 2025 wametembelea Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujenga uelewa wa pamoja kuhusu uendeshaji wa Bandari na shughuli za utekelezaji bandarini.Madiwani hao walipokelewa na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed Gallus Abed, kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa BandariĀ 
Tanzania( TPA) Bw. Plasduce Mkeli Mbossa.