MAMIA WATEMBELE BANDA LA TPA KATIKA MAONEHSO YA SABASABA KUPATA ELIMU KUHUSU SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIBNDARI

Mamia ya Wananchi na Wadau wa Bandari wamejitokeza kwa wingi katika Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ( Sabasaba) ili kupata elimu kuhusu shughuli mbalimbali za utekelezaji bandarini na kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mamlaka.