MV SEA ARIES INAENDELEA KUHUDUMIWA BANDARI YA MTWARA IKIBEBA MITAMBO NA VIFAA VYA MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA KISIWA MGAO

Bandari ya Mtwara imeendelea kuhudumia meli kutoka nchi mbalimbali ambapo tarehe 3 Julai 2025 imepokea meli ya MV SEA ARIES kutoka nchini China.
Meli hiyo imebeba tani 5,744.526 za shehena ya mizigo mchanganyiko ikiwemo magari, mitambo na vifaa kazi vya Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao.