Select your language

Kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa meli nne kubwa za mizigo katika Bandari ya Karema ni fursa kwa wananchi wa mikoa inayopitiwa na Ziwa Tanganyika ya Rukwa, Katavi na Kigoma na kuongeza kipato cha kaya na Taifa.

 

Ujenzi wa meli hizo ulianza Aprili 2025 na ukitarajiwa kukamilika Julai 2026. Mpaka sasa mradi huo umefikia zaidi ya asilimia 95 huku meli zote zikiwa majini kwa hatua mbalimbali za uhakiki wa mwisho kuanza kutoa huduma.

 

Oktoba 2023, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilipokea maombi kutoka Kampuni ya Gold Voyage Logistics Limited, kampuni tanzu ya Zijin Mining Group Co. Ltd kutoka China ikiomba kukodishwa eneo katika Bandari ya Karema ili kujenga meli hizo.

 

Hayo yamesemwa tarehe 16 Machi,2026  na Msimamizi Msaidizi wa Bandari ya Karema, Anthony Poyo na wakati wa tukio la kuingizwa majini kwa mara ya kwanza meli ya nne ambapo kukamilika michakato wa vibali ukikamilika zitatoa huduma nchi za DR Congo, Zambia, Burundi na Tanzania mnufaika mkuu kutokana na kuwa na bahari.

 

Poyo amesema kukamilika kwa meli hizo kutaimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani kama Congo, Burundi na Zambia.

 

Amebainisha manufaa ya meli hizo kwamba unatarajia kuwa na kichocheo cha usafirishaji wa madini kama ya lithium, shaba na dhahabu kutoka eneo la Manono nchini DRC yanayochimbwa na kampuni hiyo ambapo kupitia Manono, Bandari ya Kalemie hadi Bandari ya Kigoma, Dar es Salaam na Tanga zitatumika kabla ya kusafirisha Kwenda nje ya nchi.