Select your language

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed Gallus Abed ameongoza kikao cha Wadau na watumiaji.wa Bandari kilicholenga kujadili namna bora na yenye tija ya.kuanza kutumika kwa kituo cha reli ya kisasa (SGR) cha Malindi.
Kituo hicho cha Malindi kinatarajiwa kuanza kusafirisha shehena ya makasha kutoka Bandari ya Dar es Salaam kuelekea bandari kavu za Ihumwa na Isaka kwa njia ya reli.