MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI (TPA) ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO YA SABASABA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa, akiongozana na Menejimenti ya TPA, ametembelea banda la TPA katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), jijini Dar es Salaam, ambako yanaendelea Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara.Ziara hiyo imelenga kujionea namna banda la TPA linavyoendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau kuhusu huduma za kibandari, maboresho ya miundombinu, pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara zinazopatikana kupitia sekta ya bandari.

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"