MKURUGENZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM BW. ABED GALLUS ABED AMEWAONGOZA WAFANYAKAZI WA BANDARI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WAFANYAKAZI
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw .Abed Gallus Abed ameongoza Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) wa vituo vya Makao Makuu na Dar es Salaam leo kuungana na wenzao Duniani kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo yanayo kwenda na kauli mbiu "Kazi zenye staha ni nguzo imara kwa maendeleo endelevu katika utekelezaji wa dira ya Taifa 2050" alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Albert Chalamila.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"