Select your language

Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Ayubu Sebabili, amesema uwekezaji uliofanyika katika Bandari ya Tanga umeongeza chachu ya ukuaji wa uchumi katika Taifa letu.Mhe. Sebabili aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 13 ya Biashara na Utalii ya Mkoa huo yanayofanyika katika Viwanja vya Mwahako vilivyopo Jijini Tanga.“Nimekuwa nikikutana na magari ya nchi jirani za Rwanda Burundi, Zamabia, DRC , Uganda, Malawi yanatoka na kuingia bandarini hii inadhihirisha uwekezaji uliofanyika katika Bandari ya Tanga umepanua wigo wa kibiashara katika huduma za kibandari.” Aliongeza Mhe. SebabiliAwali akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya huyo Afisa Mkuu Uhusiano Bandari ya Tanga Bw. Peter Milanzi kwa niaba ya Meneja wa Bandari Bw. Salehe Mbega, alisema kuwa uwekezaji huo umefungua fursa za kibiashara katika Mkoa wa Tanga, mikoa mbalimbali nchini pamoja na nchi jirani.Pia Bw. Millanzi aliongeza kuwa uwekezaji huo umeleta mwamko mkubwa kwa watumiaji wa bandari hiyo ambapo hapo awali kabla ya maboresho nchi zinazotuzunguka zilikuwa hazitumii bandari hiyo lakini kwa sasa mpaka Zimbabwe wanatumia Bandari ya Tanga.Bandari ya Tanga inatumia jukwaa hilo kutoa elimu juu ya shughuli za kibandari, tozo mbalimbali pamoja na kutangaza fursa zinazopatikana katika bandari hiyo ambapo Kauli Mbiu ya Maonesho hayo ni “ Kuonyesha Sekta ya Kimkakati ya Mabadiriko ya Kiuchumi Kuunga Mkono Dira 2050 ya Maendeleo ya Taifa ya Tanzania”.