Select your language

Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa( Mb) ametoa wito wa kuharakisha matumizi ya mifumo ya kidijitali katika sekta ya bahari ili kuongeza ufanisi na kurahisisha biashara nchini.

 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Aprili 20,2026, wakati wa ufunguzi wa semina ya kikanda iliyolenga matumizi ya

IMO Compendium pamoja na utekelezaji wa Maritime Single Window (MSW) na mfumo wa Kidigitali wa Port Community Systems ( PCS), Prof. Mbarawa amesema,  hatua hiyo ni muhimu katika kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani.

 

Amesisitiza kuwa Bandari ya Dar es Salaam ina mchango mkubwa, ikihudumia zaidi ya 90% ya biashara ya kimataifa na nchi jirani zisizo na bandari. Maboresho kupitia mradi wa DMGP yameongeza uwezo wa bandari, huku mizigo ikifikia tani milioni 27.7 na muda wa kuhudumia meli kupungua kwa kiasi kikubwa.

 

Kwa upande wao, Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini ( IMO), wameeleza kuwa matumizi ya teknolojia si chaguo tena bali ni lazima kwa bandari za kisasa kwa kufuata miongozo, viwango na taratibu za IMO hasa usalama wa meli, usafirishaji wa mizigo hatarishi na ulinzi wa mazingira baharini.