Select your language

Serikali imesema inalenga kuitumia Bandari Kavu ya Kwala kama kichocheo cha ongezeko la mapato, kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam na hivyo kuchangia kukuza uchumi wa nchi.

 

Kauli hiyo imetolewa Aprili 29, 2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, wakati wa hafla ya kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa Bandari Kavu kwa ajili ya kuhudumia shehena ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hafla hiyo ilifanyika katika Bandari Kavu ya Kwala, iliyopo Mlandizi, Mkoa wa Pwani.

 

Prof. Kahyarara amesema kuwa uamuzi wa DRC kuanza ujenzi wa bandari yake kavu katika eneo hilo utakuwa chachu kwa nchi nyingine zilizotengewa maeneo katika Kwala kuharakisha ujenzi wa bandari zao kavu, hatua itakayoongeza ufanisi wa huduma za usafirishaji na biashara kikanda.