TPA IMEKUTANA NA WAFANYABIASHARA KUTOKA NCHINI UHOLANZI

Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Machi 11,2025 imekutana na Wafanyabiashara kutoka nchini Uholanzi katika jengo la Makao Makuu ya TPA Jijini Dar es Salaam, ili kujadiliana juu ya fursa za uwekezaji na ushirikiano wa kibiashara katika Bandari.
Ujumbe wa Wafanyabiashara hao kutoka kampuni za Invest International, Korpershoek na Ramco International ulipokelewa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt. Baraka Mdima kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Plasduce Mbossa.