TPA KUTEKELEZA MIRADI YA KIMKAKATI ILI KUVUTIA SHEHENA YA MASOKO YA NJE ZA JIRANI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema imekuwa ikitekeleza miradi ya kimkakati ili kuvutia shehena ya masoko ya nchi za jirani.
Kauli hiyo imetolewa Desemba 04 2024 na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA Dkt. George Fasha wakati akitoa mada katika Mkutano wa Tano wa Juma la Shughuli za Kibandari na Forodha unaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Dkt.Fasha amesema Bandari za Ziwa Victoria zimejengwa kimkakati ili kuvutia shehena inayoenda na kutoka nchini Uganda kutokana na ukaribu wa Kijiografia.
Aidha amesema Bandari za Ziwa Nyasa zimejengwa ili kuvutia soko la Malawi na Zambia wakati Bandari za Ziwa Tanganyika ziko kimkakati kwa ajili ya soko la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mbali na hiyo Dkt.Fasha amesema ili kujiweka karibu na Wateja wake TPA imefungua Ofisi katika nchi zote hizo zinazohudumiwa na Bandari za Tanzania.