TPA YAPOKEA TUZOYA SHUKURANI KWA KUTAMBUA MCHANGO MAMLAKA KATIKA KUFANIKISHA MKUTANO MAALUM WA MWAKA WA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ( Kulia) akimkabidhi Tuzo ya shukurani kwa kutambua mchango wa TPA kufanikisha Mkutano Mkuu Maalum wa mwaka wa Jukwaa la Wahariri ( TEF) kwa Kaimu Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA), Bw. Leonard Magomba( wa pili kushoto) ambaye alipokea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Bw. Plasduce Mbossa, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Mkuu Maalum wa mwaka wa TEF, tarehe 4 Aprili,2025 Mjini Songea Mkoani Ruvuma.
Mhe. Balozi Dkt. Nchimbi alikuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano Mkuu huo Maalumu ambapo amesisitiza umuhimu wa vyombo vya Habari katika kukuza maendeleo ya nchi. Pamoja na mambo mengine, wanahabari hao waliutumia Mkutano Mkuu huo Maalum kufanya uchaguzi wa uongozi wao mpya.