Select your language

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mha. Dkt. Baraka Mdima kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, ameshiriki hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa boti mbili za doria kwa ajili ya bahari na maziwa makuu, iliyofanyika Julai 31, 2026 Bandari ya Dar es Salaam. Boti hizo mpya, PB Sailfish 02 na PB Sailfish 03, zinaongeza uwezo wa doria baada ya uzinduzi wa boti ya kwanza, PB Sailfish, uliofanyika Machi 2, 2024. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba.