Select your language

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeshiriki kikao cha wadau kuhusu kukusanya maoni ya mapendekezo ya marekebisho ya Tozo mbalimbali za huduma za kibandari, kilichoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).

Kikao hicho cha siku moja kimefanyika tarehe 22 Desemba, 2025, mkoani Tanga, kikiwa na lengo la kuwasilisha maeneo ambayo TPA inapendekeza yafanyiwe marejeo ya tozo za huduma za kibandari, pamoja na kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja na wadau wa sekta ya bandari.

Mchakato huu muhimu ni Kikao cha Kusikiliza Maoni ya Umma, ambapo umma na wadau hupata fursa ya kutoa maoni yao kabla ya kufanyika kwa maamuzi ya mwisho.