WAFANYA KAZI WA BANDARI YA MTWARA WASHIRIKI MICHEZO MBALI MBALI
Wafanyakazi wa Bandari ya Mtwara tarehe 13 Juni, 2026 wameshiriki katika bonanza la michezo mbalimbali lililoandaliwa na Meneja wa Bandari kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi wa Bandari (DOWUTA).Bonanza hilo lililofanyika katika viwanja vya Klabu ya Bandari lilijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa kikapu (basketball), mpira wa pete (netball), mpira wa wavu (volleyball), riadha na drafti ambayo iliwapa fursa wafanyakazi kushiriki na kuonesha vipaji vyao.Akizungumzia bonanza hilo, Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi alieleza kuwa lengo kuu la bonanza hilo ni kuimarisha afya na ustawi wa wafanyakazi pamoja na kuendeleza sera ya michezo ndani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania.
Aidha, bonanza hilo limekuwa ni sehemu muhimu ya kuhamasisha wafanyakazi kushiriki shughuli za michezo na mazoezi kwa ajili ya kuboresha afya zao za kimwili na kiakili.Wafanyakazi wengi walijitokeza kwa kushiriki na kushuhudia bonanza hilo ambapo walielezea kufurahishwa na kuridhishwa na utaratibu huo wa kukutana pamoja nje ya mazingira ya kawaida ya kazi. Ushiriki huo umekuwa ni chachu ya kuimarika kwa mshikamano, upendo na ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi.Kimsingi, bonanza hilo limekuwa ni jukwaa muhimu katika kuongeza ari ya utendaji kazi wa kila siku jambo ambalo lina mchango mkubwa katika kutekeleza majukumu ya Bandari ya Mtwara na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kwa

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"