Select your language

Kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, Wanawake wa Bandari za Ziwa Victoria wakiongozwa na Meneja wa Bandari, Bi. Rosemary Ndesamburo, wameanza maadhimisho hayo kwa kutembelea watoto wenye mazingira magumu katika Kituo cha Fonelisco Children Home Centre kilichopo Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.

 

Katika ziara hiyo, wanawake hao walipata fursa ya kukaa pamoja na watoto hao, kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo pamoja na kuwapatia mahitaji mbalimbali ikiwa ni ishara ya upendo, mshikamano na kujali watoto wanaohitaji msaada katika jamii.

 

Hatua hiyo ni sehemu ya kuadhimisha siku hiyo muhimu duniani kwa vitendo, kwa kuonesha mchango wa wanawake katika kujenga jamii yenye huruma, mshikamano na matumaini kwa makundi yenye uhitaji maalum.

 

Wanawake wa Bandari za Ziwa Victoria wameendelea kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kusaidiana, kuthaminiana na kushirikiana katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii.