Select your language

Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetoa msaada wa kadi 400 za bima ya matibabu zenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa watoto wenye uhitaji maalum wanaosoma katika Shule Kumi za Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza wakati akitoa msaada huo kwa niaba ya wafanyakazi Wanawake wa vituo vya Makao Makuu na Bandari ya Dar es Salaam,Meneja Rasilimali Watu wa Bandari ya Dar es Salaam Bi.Mwajuma Mkonga amesema kutokana na changamoto za matibabu wanazopitia watoto hao TPA imeamua kuwashika mkono kwa kuwalipia bima ya matibabu jumla ya watoto 400 wa shule hiyo iliyopo katika Wilaya ya Kigamboni.

 

Alisisitiza kuwa mshikamano wa wanawake ni nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii na kuchangia maendeleo ya Taifa. Aidha, aliwataka wanawake kuendelea kujitokeza katika shughuli za kijamii na kiuchumi ili kuimarisha ustawi wa familia na jamii kwa ujumla