Select your language

Umoja wa Wanawake Wanaofanya kazi Sekta ya Bahari  Mashariki na Kusini mwa Afrika  (WOMESA) wametembelea Bandari ya Tanga na  kuridhishwa  na utendaji kazi katika bandari hiyo baada ya kukamilika kwa mradi wa maboresho ya bandari.

Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Umoja huo Mhandisi Fortunata Makoye  Kakwaya  amesema kuwa, maboresho hayo  yameleta mapinduzi makubwa katika bandari hiyo ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo meli kubwa zilikuwa haziwezi kufunga gatini kutokana na changamoto ya kina cha maji kuwa kifupi.

“Sisi Kama wadau katika sekta ya bahari maboresho haya yameleta mapinduzi makubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuifanya bandari hii ikidhi viwango vya Kimataifa katika uhudumiaji wa Meli na mizigo.

Aidha Bw. Gwakisa Mwaibuji, Afisa Mkuu Utekelezaji akiongea kwa niaba ya Meneja wa Bandari, Bw. Masoud Mrisha aliwaomba wadau hao kuwa mabalozi wazuri wa Bandari ya Tanga ili bandari hiyo iendelee kupokea shehena kubwa zaidi na mapato makubwa.