WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI ATEMBELEA OFISI YA TPA NCHINI MALAWI

Matukio mbalimbali katika Picha wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, alipotembelea Ofisi ya TPA Jijini Lilongwe nchini Malawi hivi karibuni.
Mhe. Balozi Kombo, ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kazi kubwa inayoifanya katika kuendeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo kupitia Sekta ya Bandari.
Katika ziara yake hiyo Mhe. Balozi Kombo aliambatana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt. Baraka Mdima.