Watumishi Wanawake wa Bandari ya Mtwara wameungana na wanawake wote Duniani katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika Viwanja vya Mashujaa vilivyopo Mjini Mtwara.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Abdallah Mwaipaya ambaye ametoa wito kwa Wanawake wote kuungana katika kushiriki shughuli za maendeleo.