KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA (PIC) YAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imeipongeza Serikali ya Awamu ya sita kwa ufanisi mkubwa wa kiutendaji unaonekana katika Bandari ya Dar es Salaam, uliochagizwa na uwekezaji wake mkubwa katika miundombinu ya Bandari.Akizungumza mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam, tarehe 23 Mei,2026, Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe. Masanja Kadogosa( Mb), amesema Kamati imeridhishwa na maendeleo makubwa ya uwekezaji katika miundombinu yanayoendelea bandarini hapo, ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika kuendesha Bandari hiyo, ambayo yameongeza kasi ya uhudumiaji wa Shehena kwa kiwango kikubwa. Kamati hiyo pia imempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake katika maboresho ya miundombinu ya bandari ambayo hatimaye yanachangia kuimarisha mchango wa bandari hiyo katika uchumi wa Taifa.Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof.Makame Mbarawa (Mb), ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ( PIC) kwa kufanya ziara hiyo ambayo imewapa fursa yakujionea kazi kubwa inayotekelezwa na Serikali katika kuimarisha sekta ya bandari nchini.Mhe. Prof. Mbarawa amesema Serikali itaendelea kuwekeza Katika maboresho ya miundombinu ya bandari pamoja na mifumo ya kisasa ya uendeshaji na kushirikisha Sekta Binafsi katika uendeshaji ili kuhakikisha bandari za Tanzania zinaendelea kuwa kitovu muhimu cha biashara kwa nchi za Ukanda wa Afrika mashariki, maziwa Makuu na kusini mwa Afrika.
Mhe. Prof. Mbarawa pia ameihakikishia Kamati kuwa maoni, ushauri na maelekezo yote yaliyotolewa wakati wa ziara hiyo yatafanyiwa kazi kwa lengo la kuongeza zaidi ufanisi wa huduma bandarini na kuimarisha mchango wa sekta ya bandari katika kukuza uchumi wa Taifa.Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) Bw. Plasduce Mbossa, ameileza Kamati kuwa TPA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na maboresho ya miundombinu ili kuongeza uwezo wa kuhudumia mizigo mingi zaidi kwa wakati na kufafanua kuwa maboresho hayo yamechangia kuongezeka kwa mapato ya ndani ya mamlaka hiyo pamoja na kuimarika kwa ushindani wa bandari katika kuhudumia masoko ya nchi jirani zinazotegemea Bandari ya Dar es Salaam kama lango kuu la biashara.
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"