KAMATI YA MABORESHO YA BANDARI IMEKUTANA KATIKA KIKAO CHAKE CHA 33

Kamati ya Maboresho ya Bandari (Port Improvement Committee - PIC) inayojumuisha Wadau wa Sekta ya Uchukuzi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, imekutana katika kikao chake cha 33 kilichofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA ) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara, ameipongeza TPA kwa kuendelea kuboresha utendaji unachangia kuongeza ufanisi wa sekta nzima ya Uchukuzi nchini, ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa malori kuingia na kutoka bandarini na mchakato mzima wa usafirishaji wa shehena.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw Abed Gallus Abed, alisoma taarifa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam na kueleza kiwango cha shehena iliyohudumiwa imekuwa ikiongezeka kwa kiwango cha wastani wa asilimia 15 kila mwaka.