KATIBU MKUU PMAESA AMEKUTANA NA MENEJIMENTI YA TPA KATIKA KIKAO KILICHOLENGA KUIMARISHA MAHUSIANO

Katibu Mkuu wa Chama cha Usimamizi wa Bandari Mashariki na Kusini mwa Afrika (Port Management Association of Eastern and Southern Africa-PMAESA) Kanali Andre Didace Ciseau amekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kikao kilicholenga kuimarisha uhusiano baina ya pande hizo mbili.
Kanali Ciseau amesema PMAESA inatambua na kuthamini mchango wa TPA kama miongoni mwa taasisi zenye uwezo mkubwa kiutendaji katika Ukanda wa Kusini na Mashariki mwa Afrika.
Akizungumza katika Kikao hicho Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt. Baraka Mdima ameeleza mipango ya muda mfupi na mrefu ya TPA na utayari wa Mamlaka kuendelea kuimarisha ushirikiano wake na PMAESA.