Kikosi cha Zimamoto na Usalama Bandari ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na  vikosi vya uokozi vya  kiserikali na binafsi  leo tarehe 22 Mei , 2025 limefanya zoezi la  utayari wa kukabiliana na majanga ya moto lililofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam. 

Meneja zimamoto na Usalama Bw. Mussa Biboze akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed amesema kuwa zoezi hilo  limefanyika kwa ufanisi  mkubwa  kwa kuwa wameweza kuudhibiti moto huo kwa muda mfupi zaidi wa dakika 15 tu. 

Aidha amesema kuwa zoezi hilo lililenga kupima utayari katika mashirikiano ya vikosi vya uokozi  iwapo itatokea majanga ya moto 

Zoezi hilo  limehusisha vikosi vya uokozi ambavyo viko chini ya TPA , vikosi mbalimbali vya usalama kama jeshi la zimamoto, Wanachi, Polisi pamoja na makampuni binafsi yanayojishughulisha na kuzima moto, huduma za dharula za uokozi na hospitali ya Taifa Muhimbili .