MKUU WA MKOA AHAHIDI OPERESHENI MAALUMU KUONDOA FOLENI YA MALORI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, ameahidi kuendesha operesheni maalum ya kuondoa tatizo la foleni katika njia kuu zinazotumika kusafirisha shehena kutoka Bandari ya Dar es Salaam, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa bandari na kuboresha mtiririko wa usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya jiji. Mhe. Chalamila ametoa kauli hiyo leo, tarehe 29 Julai 2026, alipotembelea mzani wa kupima uzito wa malori yanayosafirisha shehena kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda bandari kavu na maeneo mbalimbali nchini. Mzani huo unasimamiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Amesema Serikali ya Mkoa itachukua hatua za haraka kushughulikia changamoto zinazochangia msongamano wa magari, hususan katika maeneo ya mizani na sehemu zinazotumika kuhifadhi malori kando ya barabara, ili kuhakikisha usafirishaji wa shehena unakuwa wa haraka, salama na wenye tija zaidi. Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam katika mnyororo mzima wa usafirishaji wa shehena, kupunguza muda wa kusafirisha mizigo na kuondoa adha ya foleni ambayo imekuwa ikiathiri shughuli za biashara na usafirishaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed G. Abed, amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa Integrated Weighbridge, utakaounganisha mzani wa TANROADS na mfumo wa Bandari ya Dar es Salaam. Amesema mfumo huo utawezesha malori kupimwa mara moja badala ya kupitia hatua nyingi, hivyo kupunguza foleni, kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma na kuhakikisha mizigo inawafikia wateja kwa wakati.
Utekelezaji wa hatua hizi unatarajiwa kuimarisha zaidi ushindani wa Bandari ya Dar es Salaam kama lango kuu la biashara na usafirishaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.“Tumekuja kujionea kazi inayofanywa na TAEC hapa bandarini, kwa kuwa ndiyo taasisi yenye jukumu la kutoa leseni za matumizi ya Midaki pamoja na kutoa mafunzo kwa watumiaji wa vifaa hivi. Tumejiridhisha kuwa matumizi ya Midaki yanafanyika kwa usalama na kwa kuzingatia viwango vinavyolinda afya ya wafanyakazi na madereva wanaopita katika maeneo ya ukaguzi,” alisema Prof. Msambichaka.
Aliongeza kuwa matumizi ya teknolojia ya Midaki zinazotumia mionzi yameleta mapinduzi katika ukaguzi wa mizigo kwa kuongeza kasi ya utoaji wa huduma, kupunguza muda wa ukaguzi na hivyo kuchochea ufanisi wa biashara na maendeleo ya uchumi. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Usalama wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Dkt. Jumanne Fhika, alisema Mamlaka kwa sasa inatumia jumla ya mashine za skana 11 katika bandari zake, hatua inayochangia kuharakisha ukaguzi wa makasha, kuboresha utoaji wa huduma na kuongeza mapato ya Serikali. Alisema uwekezaji unaoendelea kufanywa na TPA katika teknolojia za kisasa za ukaguzi ni sehemu ya mkakati wa kuongeza ufanisi wa shughuli za bandari, kuimarisha usalama wa mizigo na kuwezesha biashara kufanyika kwa haraka zaidi. Katika ziara hiyo, wajumbe wa Bodi ya TAEC walitembelea moja ya vituo vya ukaguzi wa makasha kwa kutumia Midaki katika Bandari ya Dar es Salaam na kujionea hatua mbalimbali za ukaguzi zinavyotekelezwa kwa kutumia teknolojia hiyo ya kisasa
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"